HATIMA YAKO
TUMIA LEO YAKO ILI UTENGENEZE KESHO YAKO NZURI AU HATIMA YAKO
✍Mwalimu na mwandishi
ππππ
Fredrick kapaya
Mhubiri 7:8
"Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi"
Ecclesiastes 7:8
"The end of anything is better than its beginning.... "
Maana ya neno Hatima ni sawa na kusema mwisho
πElewa kuwa kila jambo huwa lina mwanzo wake na mwisho wake.
πMwanzo wa jambo unaweza ukawa mzuri au mbaya na mwisho wa jambo unaweza ukawa mzuri au mbaya.
πMwisho mbaya au mzuri unaweza ukachangiwa sana na mwanzo wa hilo jambo (ulianzaje?)
πMtu anaweza kuokoka na kuishi maisha ya wokovu ila akafa katika dhambi, hiyo hatima mbaya.
Isaya 46:10
"Nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado, nikisema shauri langu litasimama, nami nitatenda mpenzi yangu yote"
Isaiah 46:10
"From the beginning i predicted the outcome,.... "
➡Mungu alipotuumba tayari ameshatuwekea hatima zetu, ila shetani anaweza kuharibu hatima ikawa mbaya.
Jambo la msingi sana
▶Ukifanya mambo sawasawa na kusudi la Mungu na kuishi maisha matakatifu hakika utakuwa na uwezo wa kuifikia hatima nzuri (mwisho)
Ufunuo 14:13
"Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumnzika baada ya taabu zao, kwa kuwa matendo yao yafuatana nao"
➡Kwa tafsri hiyo hali ya kumcha Mungu katika roho na kweli husababisha ufikie hatima nzuri, kutomcha Mungu au kuwa mnafiki kunatengeza hatima mbaya.
Mhubiri 12:1
"Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, mimi sina furaha katika hiyo "
πͺπͺLeo yako inanguvu kubwa ya kutengeza kesho itakuwaje. Unachofanya leo kizuri au kibaya kinaweza kikatengeza mwisho uwe mzuri au mbaya.
✍Mwanadamu huzaliwa, hukua na huwa mtu mzima hatimaye huzeeka.
➡Katika eneo la ujana ndilo unaweza ukalitumia sana kutengeneza kesho yako, kwa sababu unapokuwa kijana unakuwa na nguvu za kufanya kazi, au kufikiri.
Mithali 20:29
"Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi"
➡Ukitumia eneo la ujana vizuri unaweza kutengeneza uzee mwema. Tumia ujana wako vizuri ujifunze kuwa na hekima ili ukizeeka uwe mzee mwenye hekima.
Lakini nikienda mbali zaidi kibiblia
πKila mtu analeo yake ila hakuna anayeijua kesho, ila tunaweza kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya kesho ikawa nzuri.
πUwapo mzima tumia wakati vizuri kuutafuta uso wa Mungu pasipo kuchoka, ishi ukijua ya kuwa una mwisho wako.
Mwalimu Fredrick kapaya
Kapayafarajaph@gmail.com
0768226595
Mungu akubariki sana
Comments
Post a Comment