UAMINIFU
💡 SOMO: JIFUNZE KUWA MWAMINIFU KATIKA MAISHA YAKO
Na
Mwl Fredrick Kapaya
E-mail: kapayafarajaph@gmail.com
My Missio is to teach the WORD OF GOD to all people.
Nina kusalimu katika Jina la Yesu mwana wa Mungu aliye hai karibu tujifunze neno.
Ufunuo 2:10
_"Usiogope mambo yatakayokupata, tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. *Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima*"_
✍️ Katika maisha kuna vitendo vikubwa vitatu ambavyo mtu huweza pitia mpaka kufikia hatima yake.
👉 *Kuanza* jambo
👉 Kuendelea kufanya jambo
👉 Kufikia hatim au mwisho wa jambo.
[Kuzaliwa, kuishi na kufa]
👉Eneo ninaloliwinda ni eneo la *kuishi* kwa sababu ndiko hutoa hatima ya mtu baada ya kufa kwake.
*Mhubiri 7:8a*
_"Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake"_
🔘 Wapo baadhi ya watu ambao katika maisha yao hapa duniani walikuwa na record nzuri, wengine walikuwa ni wahubiri wazuri, wengine walikuwa ni waimbaji wazuri sana, wengine walikuwa ni wanamaombi wazuri lakini kwa sababu ya kutokuwa *waaminifu katika utumishi wao* mwisho wao ulikuwa mbaya.
*Ezekiel 18:24*
_"Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo... "_
🔹Lakini pia wapo ambao walionekana kuwa ni watu wenye dhambi sana lakini mwisho wao ulikuwa mzuri.
👆👆Kwa sababu hiyo upo uwezekano kabisa wa mtu *kuanza jambo vizuri* ila *anaweza kumaliza vibaya*.
👉Mara nyingi sana kinachoweza kuashiria mwisho mbaya wa mtu ni namna anavyoendelea katika jambo fulani / namna anavyoenenda au mwenendo wa mtu husika.
💡Kinachoweza kutoa matokeo halisi ya kile ulichokuwa unakifanya ndani ya utumishi wako ni mwisho wako {Tukifika kwenye kiti cha hukumu haijalishi ulikuwa mtumishi, mwimbaji nk lakini utahukumiwa sawasawa na matendo yako halisi uliyokuwa ukifanya}
🔹 Fanya yote katika dunia hii kwa siri huku ukiwa umevaa sura ya utumishi ila ndani yako kaa ukielewa kuwa mwisho wako unakuja [Ndiko kutakuwa na kilio na kusaga meno].
*1 Wakorintho 9:26-28*
_"Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo si kama asitaye, napigana ngumu vivyo hivyo, si kama apigaye hewa, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha, isiwe, nikiisha *kuwahubiri wengine mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa*"_
👉Katika mazingira mengine kuanza jambo inaweza kuwa ni rahisi sana ila shida inaweza kuja kwenye *kuendelea* vizuri mpaka kufikia hatima yako.
💡Wengine wanapoanza jambo huwa na walimu ambao huwapa maelekezo ya namna ya kuenenda ila tatizo huja pale mtu anapozoea na kujiona kuwa anajua zaidi ya mwalimu wake hapo ndipo kiburi huinuka.
👆Mwenendo hubadilika kisha hatima au mwisho wa mtu huwa ni mbaya sana.
*Unaweza kujiona kuwa unajua sana kumbe bado haujui kile unachopaswa kujua katika nyakati ulizopo*
*Mfano*: Kuokoka linaweza kuwa ni jambo jepesi sana kwa mtu ila shida huja kwenye eneo la namna ya kuishi ndani ya huo wokovu.
💡Baadhi ya wakristo wamekosa *uaminifu* kabisa katika maisha yao ya wokovu. Kukosa uaminifu hupunguza sifa ya mtu kuupata uzima wa milele.
🧠Baadhi ya watu walipookoka na kuanza safari ya maisha ya wokovu, walikuwa na hofu ya Mungu (waaminifu mbele za Mungu) lakini walipozoea wokovu *wengi wamepoteza uaminifu mbele za Mungu*
Biblia inasema kuwa:
*Uwe mwaminifu mpaka kufa*
👆Katika maisha yako yote hakikisha una kuwa mwaminifu katika mambo yote mbele za watu na mbele za Mungu.
🔊 Usipokuwa mwaminifu elewa kuwa kazi unayoifanya ni bure kabisa {hamna kitu kinachoweza kukuumiza sana kama unafanya kazi fulani kwa bidii halafu mwisho wake unaambiwa haujafanya chochote kazi yako ni bure }
👉Paulo anawaambia Wagalatia.
*Wagalatia 3:3-4*
_"Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho mnataka kukamilishwa sasa katika mwili? Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli"_
👆Paulo aliujua vizuri mwanzo wao
👉Lakini anao mwenendo wao unaashiria mwisho mbaya.
💡Utumishi wako usiwe bure, ukristo wako usiwe bure. Hakikisha unakuwa mwaminifu ili kazi yako na mateso uliyoyapata katika utumishi wako yasiwe bure.
*Wafilipi 3:12-14*
_"Si kwamba nimekwisha kufika au nimekwisha kuwa mkamilifu, la Bali *nakaza mwendo ili nipate* kulishika lile ambalo kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo...... 14. *nakaza mwendo niifikilieii mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo*"_
*Yesu akubariki*
Comments
Post a Comment