KUFIKIA MALENGO
SOMO:
MAMBO YATAKAYOKUSAIDIA UFIKE UNAKOTAKA KUFIKA KWENYE MAISHA YAKO YA KIROHO NA
KIMWILI AU UYAFIKIE MAFANIKIO YAKO ULIYOYAWEKA KWENYE MAISHA
Lengo la somo
Ni kukuonesha kuwa
katika safari yoyote ile unayoianzisha kwenye maisha yako ili ufike salama
unakotaka kufika unahitaji maandalizi
mazuri au yakutosha, mikakati yenye nguvu na ramani itakayokuelekeza
kufika unakotaka kufika, lakini pia unahitaji imani yaani uamini kwamba
utafika unakotaka kufika.
Utangulizi
Watu
wengi Sana kwenye dunia hii, huwa Na malengo kwenye maisha Yao yawezekana
malengo ya biashara, kwenye huduma, familia au jambo lolote lile. Haitoshi tu
kuwa na malengo ila hutamani kuyafikia hayo malengo au kufikia kiwango
wanachotaka kufika. Wengi huweza kukwama kufika wanakotaka kufika kwa sababu ya
kusikiliza sana sauti za duniani ambazo huwafanya kujijengea mitazamo hasi au
wengine hukwama kwa sababu ya mikakati mibovu na isiyo na nguvu ya kuwafikisha
wanakotaka kufika.
Mambo yatakayokusaidia kufika
unakotaka kufika au kuyafikia malengo unayotaka kuyafikia kwenye maisha yako ya kimwili na kiroho.
- Ili ufike unakotaka kufika unahitaji nguvu za Mungu zitokanazo na chakula cha rohoni (Neno la Mungu) na uhakika wa kutosha ndani yako wa kufika unakotaka kufika kwa msaada wa Roho Mtakatifu.
1 Wafalme 19:4
“Lakini yeye mwenyewe akaendelea
katika jangwa mwendo wa siku moja , akaenda
akaketi chini ya mretemu .Akajiombea
roho yake afe ,akasema ,Yatosha ,sasa, Ee BWANA ,uniondoe roho yangu ; kwa
kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu .Naye kajinyosha akalala chini ya mretemu;
na tazama malaika akamgusa ,akamwambia ,inuka ule”
1 Wafalme 19:7
“Malaika wa Bwana akamwendea mara
ya pili, akamgusa akasema, inuka, ule,
maana safari hii ni kubwa mno”
Baada
ya Eliya kuwaua wale manabii wa Baali na kupata vitisho vya kuuliwa Eliya
aliingiwa na hofu sana. Eliya alikimbia ili aiokoe roho yake kwa sababu
Yezebeli alitafuta kumuua, yawezekana ndani yake alikuwa amekusudia kufika eneo
ambalo litakuwa na usalama au eneo ambalo adui hata weza kufika kwa ulahisi.
Lakini
alipokuwa kwenye hiyo safari kuna mambo yalimtokea ndani yake, jambo la kwanza alihisi
kukata tamaa ya kufika alikokuwa anataka kufika“Akajiombea roho yake afe, akasema,
Yatosha, sasa, Ee BWANA, uniondoe roho yangu”,
Jambo la pili;
aliishiwa nguvu za kuendelea
alikukuwa anaenda.
“Lakini
yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi
chini ya mretemu”
Yawezekana
hata wewe kuna eneo au kituo fulani kwenye maisha yako umekaa kwa mda mrefu
sana na umejikuta ukijitamkia maneno ya kuchoka na kukata tamaa ya kuendelea
mbele au kuishiwa nguvu.
Kukaa kwenye kituo fulani au jambo fulani kwa mda mrefu pasipo
kuendelea mbele, yaani unatumia nguvu kubwa sana kwenye
jambo fulani lakini haufiki unakotaka kufika au unapata matokeo madogo,katika
hali hiyo ni wakati mzuri sana ambao marafiki waliokutia moyo wakati unaanzisha
jambo fulani kukukimbia na kukudharau.
Ukiona
hivyo elewa ya kuwa unahitaji sana ufahamu
na nguvu za Mungu kuja ndani yako ili zikusaidie uweze kufika unakotaka kufika,
Nguvu hizi na ufahamu huu wa kimungu unapatikana kwa kula chakula cha kiroho.
Eneo
hili linahitaji usikivu sana ndani yako na hali ya kufanya au kutekeleza
maagizo ya kuinuka na kula chakula, huku ndani yako ukijua ya kuwa bado
unasafari ndefu sana kwa hiyo unahitaji kula chakula cha kutosha ili upate
nguvu ya kukusaidia kufika unakotaka kufika.
Elewa
ya kuwa Mungu tayari kakuandalia chakula cha kukupa nguvu ya kufika unakotaka kufika,
chakula hiki unaweza kukipata kupitia mafundisho mbalimbali ya neno la Mungu,
lakini tatizo linaweza likawa ndani ya mtu kuwa na upofu wa kiroho au kukosa
ufahamu au kwa sababu ya kukata tama tumeshindwa kukiona chakula
alichotuandalia Mungu.
Wakati
ambapo Eliya alikuwa amechoka na kutamani kufa, ndio ulikuwa wakati ambao Mungu
aliachilia chakula kwa Eliya, lakini kama ingetoke Eliya asingekuwa na usikivu
wa kuinuk inamaa asingeona chakula lakini angeshindwa kufika alikokuwa anataka
kufika.
1
Wafalme 19:6
“Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la
maji, kichwani pake .Akala akanywa, akajinyosha tena”
Lakini
pia upo wakati tunakula chakula katika wakati fulani (neno la Mungu) lakini
tumekosa kuwa na ufahamu wa kujua sababu ya kula hicho chakula, matokeo yake
tunakula lakini bado tunaendelea kukaa kwenye hicho kituo.
Malaika
alimwendea tena Eliya kumsisitiza ale, yawezekana alikula kidogo kwa sababu
hakujua ya kuwa alikokuwa anaenda ni mbali, kwa sababu hiyo Malaika alitaka
Eliya ale ili asichoke njiani na afike ambapo alitakiwa kufika.
1
Wafalme 19:7
“Malaika wa BWANA akamwendea mara
ya pili, akamgusa akasema, inuka, ule;
maana safari ni kubwa mno kwako”
1
wafalme 19:8
“Akainuka, akala, akanywa, akaenda Kwa nguvu za chakula hicho siku
arobaini mchana Na usiku hata akifika Horebu, mlima wa Mungu”
Nguvu
ya chakula (Neno) inaweza kukusaidia kufika unakotaka kufika, kama tu ukiamua
kufutilia na kuchukua maamuzi ya kujifunza neno kwa hali ya juu ili likusaidie
katika safari yako ya kufikia jambo fulani kwenye maisha yako lakini pia
kuufikia uzima wa milele.
Jambo
la msingi sana; Jitahidi sana unapoanza safari ya
kufikia jambo lolote lile kwenye maisha yako ,tafuta kwanza kujua uhakika wa nguvu iliyondani yako ya kukuwezesha
kufika unakotaka kufika , kama ukikosa uhakika
wa kulifikia hilo jambo ni vyema ukaacha kwenda au kulianzisha hilo
jambo. Kaa na Mungu vizuri mpaka upate uhakika wa kutosha juu ya hilo jambo.
Na
ikitokea umepata uhakika ndani yako kupitia Roho Mtakatifu, basi hakikisha
unafanya au unaendelea mbele ili ulifikie au ufike unakotaka kufika pasipo
kuangalia ulipotoka au sauti nyingi za watu, kwa sababu ukingalia nyuma kuna
uwezekano wa wewe kujiona kuwa haustahiri kufika huko.
Wapo
watu watakao inuka na kukutia moyo unapoanza safari (kimaisha, kiimani, ndoa,
mahusiano na mambo mengine), lakini pia wapo wangine wapo kwa ajiri ya
kukukatisha tamaa. Maneno ya watu yapo ndugu yangu na kelele nyingi sana za watu,
kelele hizi huweza kuongezeka sana.
Acha
kusikiliza sana maneno ya watu wanasema nini juu yako kwa ajili ya kukukatisha tamaa
ila sikiliza nini Mungu anasema juu yako.
Pata nakala ya kitabu cha somo hili
kwa mawasiliano 0768226595
kapayafarajaph@gmail.com
Mwl Fredrick kapaya
Mungu akubariki sana
Comments
Post a Comment