SOMO: MAFANIKIO
Mwl: Fredrick Kapaya
E-mail: Kapayafarajaph@gmail.com
Malengo ya somo:
Malengo ya somo:
- Ni kukusaidia kujua kuwa mafanikio yako mengi ya kimwili huanzia kwenye ulimwengu wa roho au kuzuiliwa rohoni.
- Kukusaidia kujua kuwa mafanikio yako mengi ya kimwili huanzia kwenye ulimwengu wa roho au kuzuiliwa rohoni.
- Kukujengea kiu ya kuimarisha uhusiano wako na Mungu ili ufanikiwe mwilini na rohoni.
- Kukusaidia kujua vizuizi vilivyopo kwenye ulimwengu wa roho vinavyozuia wewe usifanikiwe kiroho na kimwili.
Utangulizi:
Mwanadamu yeyote yule aliyeumbwa na Mungu katika dunia hii, ndani yake huwa na kiu ya kufanikiwa katika mambo au jambo lolote lile analolifanya au atakalo lifanya. Wakati mwingine wapo watu ambao wanashindwa kufanikiwa kwenye maeneo mbalimbali kwenye maisha yao kwa sababu ya kukosa ufahamu wa kutoshwa wa kujua nini maana ya mafanikio, kwa sababu hiyo wapo wengine ambao wanadhani wamefanikiwa kabisa na hata watu wengine wakiwaona wanaona kweli wamefanikiwa ila kumbe kwa uhalisia wanakuwa bado hawajafanikiwa kimaisha.
3 Yohana 1:2
"Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo"
Swali la ufahamu
Je kwenye maisha yako ya rohoni na mwilini umefanikiwa? na kama umefanikiwa nini kinakupa ujasiri wa kusema umefanikiwa?
Maana ya mafanikio
Kufanikiwa au mafanikio ni hali ya mtu kuyafikia malengo yake aliyojiwekea kwenye maisha yake. Kama kuna malengo kwenye maisha yako umejiwekea na ukayafikia basi wewe ni mtu mwenye mafanikio, kwa tafsri hiyo mtu ambaye hayafikii malengo yake ni mtu ambaye hajafanikiwa.
Jipatie nakala ya kitabu hiki
0768226595
0768226595
Mungu akubariki sana

Comments
Post a Comment