UNAWEZA KUTENGENEZA, KUTENGENEZEWA AU KUNUNUA MATATIZO KWENYE MAISHA YAKO
✍ Mwalimu na mwandishi
Fredrick kapaya
๐
➡ Unaweza kujitengenezea wewe mwenyewe matatizo kwenye maisha yako au kutengenezewa na watu wengine kwa kujua ama kwa kutokujua lakini pia unaweza nunua matatizo au tatizo.
๐Tatizo linaweza nunuliwa na mtu kwa kutumia(kihelehele, huruma nk) vilivyondani ya Mtu.
Wengi wakiisha yanunua haya matatizo.
1⃣ Huyachukua kwa kujua ama kwa kutokujua
2⃣ Huyaweka kwenye mifumo ya maisha yao
3⃣ Huyamiliki kama yao Kabisa bila ya kuyachunguza kwa makini.
4⃣ Huanza kushughurika nayo matokeo yake huingia kwenye mtego na hayo matatizo huanza kuwaathiri katika hali zao za kimaisha.
๐๐
Simaanishi kuwa usishughulike na matatizo ya watu ila jifunze kuyapima kwanza kabla ya kushughulika nayo kiundani kabisa ikiwezekana hakikisha mwenye tatizo anakueleza ukweli juu ya tatizo lake isije nawe ukaingia kwenye tatizo wote mkawa ndani akakosekana wa kumsaidia mwenzake.
Ni muhimu uelewe kuwa
๐ Maisha yetu yamekaa kwenye mifumo fulani ambayo kwa kweli huweza kusababisha sisi wenyewe tujitengenezee, kutengenezewa au kununua matatizo.
๐♀Hatuwezi tukaikimbia hii mifumo kwa sababu ipo tu ila tunaweza kutengeneza mazingira yatakayotusaidia kupunguza athari hizo.
Jambo la ufahamu la kutafakari
➡ Angalia unafanya nini sahvi kwa ajiri yako mwenyewe, watu wengine wanafanya nini kuhusu wewe, wewe unafanya nini kuhusu watu wengine.
๐Kinachofanywa kina faida zipi na hasara zipi? Kwako na kwa wengine.
๐Je hicho unachofanya kinachofanywa kinaulazima wa kufanya wakati huo.
✍ Kujitengenezea matatizo
Mifano:
๐๐๐๐บKula ni jambo zuri na kila mtu hupenda, ila kula sana(Ulafi) sio jambo zuri na hata Mungu hapendi. Kwa sababu hiyo mtu anaweza kuvimbiwa au kuumwa tumbo kwa sababu ya kula kupita kiasi.
๐Tatizo la kuumwa tumbo utakuwa umelitengeneza wewe mwenyewe.
๐ Tatizo linaweza kuja likaingia kwenye maisha yako kisha likaanza kukutafuna polepole au halaka halaka hatimaye kuhalibu maisha yako au ikitokea limeondoka basi litakuachia mambo kadhaa.
๐Funzo
๐Maumivu
๐Uharibifu wa kifikra au kuwa na mitazamo hasi juu ya watu.
Kapayafarajaph@gmail.com
Mwl Fredrick kapaya
Mungu akubariki
Comments
Post a Comment