UPENDO
USIBEBE CHUKI MOYONI MWAKO ILA BEBA UPENDO
Walawi
19:17
"Usimchukie ndugu yako moyoni mwako, ni lazima
kumkemea jirani yako, wala usichukue dhambi kwa ajili yake usifanye kisasi, wala kinyongo juu ya wana wa watu wako, bali umpende
jirani yako kama nafsi yako, mimi ndimi BWANA*"
- Maana ya neno chuki
Chuki ni hali ya kutompenda mtu au watu au hali
ya kuwa na roho mbaya, Chuki pia inaweza kuwa ni hali ya kugombanisha watu,
fitina au kukasirika.
Mambo ya
msingi kwenye hili somo
➡ Chuki
inaweza kutengenezwa na mtu au watu kwa sababu zao wanazozijua wao wenyewe
zinaweza kuwa za msingi au zisiwe za msingi.
➡Moyo
huweza kupenda au kuchukia, kwa sababu hiyo upo wakati mtu hupenda na upo
wakati mtu huchukia.
Mhubiri
3:8
"Wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia....."
- Upo wakati unaweza kuchukia au kuchukizwa na mtu au watu ila hakikisha usiiweke chuki ndani yako.
➡Wapo
watu wanaokuchukia (hawakupendi) ila wewe haujui kama wanakuchukia.
Zaburi
69:4
"Wanaonichukia
bure ni wengi kuliko nywele za kichwa changu"
➡ Chuki
ni tabia inayoweza kukusababishia wewe usiurithi uzima wa milele
❤ Moyo
huweza kubeba upendo juu ya watu au mtu lakini pia moyo unaweza kubeba chuki
juu ya mtu au watu.
✍ Moyo
ukibeba chuki kwa mda mrefu huweza kuharibika, kuchafuka, kupoteza tabia fulani
za upendo.
πUtachoka
kwa sababu chuki ni mzigo mzito sana moyoni, ukichoka moyo matokeo yake unaweza
kufanya maamuzi mabaya yatakayokugharimu wewe na ndugu zako.
- Chuki inaweza kusababisha mtu awaze mabaya juu ya mtu mwingine.
Mwanzo
27:4
"Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ule
mbaraka babaye aliombarikia. Esau akasema moyoni mwake, siku za kumlilia baba
yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua
ndugu yangu Yakobo”
❤
Ukibeba upendo hautachoka kwa sababu upendo huleta wepesi ndani ya moyo ila
elewa kuwa upendo unagharama. Ukitaka upendo ukae ndani yako au uwapende
wengine kubali kuingia gharama
πMungu
aliingia gharama ya kumtoa mwana wake wa pekee ili afe kwa ajiri yetu.
kwanini
aliingia gharama?
- Kwa sababu alitupenda mno.
Yohana
3:16
"Kwa maana kwa jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee...."
π
Mtu akibeba chuki juu ya rafiki yake au ndugu yake basi hawezi au
hataweza kusema naye kwa amani.
π
Na hata kama akisema naye basi ataongea naye tu kwa sababu
imembidi ila kule ndani kutakuwa hakuna amani kabisa wala furaha ya kuendelea
kusema naye.
Mwanzo
37:4
"Ndugu
zake wakaona ya kuwa baba yao anampenda kuliko ndugu zake wote, wakamchukia,
wala hawakuweza kusema naye kwa amani"
- Usifurahie au kukubari kuendelea kuwa na hiyo hali ya kukosa amani na huyo mtu au watu ila Biblia inasema Kuwa.
Waebrani
12:14
"Tafuteni
kwa bidii kuwa na amani na watu wote.... "
1 Yohana
2:9-11
"Yeye asemaye kwamba yupo nuruni, naye
amchukia ndugu yake, yumo gizani hata
sasa. Yeye apendaye ndugu yake, akaa
nuruni ,wala ndani yake hamnakikwazo"
π
Chuki ikibebwa sana moyoni huwa kama ufunguo unaofungua mlango wa kuruhusu giza
kuingia moyoni mwako.
π
Upendo ni ufunguo unaofungua mlango kuruhusu Nuru kuingia Ndani
ya moyo wa Mtu.
πͺ
Chuki ni kisu kikali sana ikiingia kanisani au katika kundi la
watu, huligawa haraka sana kundi na kutengeneza matabaka makubwa Sana.
✍Chuki
inaweza isiletwe na watu kwenye kundi la watu ila inaweza kuletwa na mtu kwenye
kundi la watu.
1 Yohana
4:20
"Mtu
akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo, kwa maana
asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye
hakumwona"
π
Haupaswi kabisa kuwa na chuki ndani ya moyo wako au kuwachukia
wanaokuchukia ila unawajibu wa kuwapenda wanaokuchukia.
✍Endapo
utakuwa na chuki halafu unasimama kuhubiri, kuimba, kuomba, basi elewa kuwa
kwakweli bado haujamjua vizuri Mungu unayemwabudu.
1 Yohana
4:7
"Wapenzi, na mpendane, kwa kuwa pendo latoka
kwa Mungu, ni kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa hakumjua Mungu, kwa maana
Mungu ni pendo”
Usimchukie ndugu yako ila mpende.
1 Yohana
3:15
"Kila
amchukiae ndugu yake ni mwuaji : nanyi mnajua ya kuwa kila- mwuaji hana uzima
wa milele ukikaa ndani yake"
Mwl Fredrick kapaya
0768226595
Luka 6:27
Mungu akubariki sana
Comments
Post a Comment