USIKATE TAMAA
SOMO: USIKATE TAMAA UNAPOPITA JANGWANI
✍ Mwalimu na mwandishi
๐๐๐๐
Fredrick kapaya
๐
Kumb 1:19
"Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama Bwana Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea"
Mambo ya msingi ndani ya hili somo
๐Kila mtu kwenye maisha haya hupitia hali fulani ngumu katika kipindi fulani cha kimaisha.
๐Unapokuwa jangwani(kwenye hali ngumu) haupaswi kumuacha Mungu.
Ayubu 1:22
"Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi, wala hakumwazia Mungu kwa upumbavu"
๐Unapokuwa kwenye shida fulani haupaswi kuacha unachokifanya kwa ajiri ya Bwana (kuacha kusali au kwenda Ibadani)
๐Elewa ya kuwa si wewe tu ni wa kwanza kupita jangwani ila wapo waliopita na wakavuka kisha wakifika salama.
๐Usipoteze mda wako mwingi kunung 'unika na kuwalaumu watu kutokana na shida ulizonazo ila tumia mda wako mwingi kufikiri zaidi juu ya kutoka kwenye hiyo shida.
๐ Elewa ya kuwa Mungu anakusudi la kukutoa eneo moja la kimaisha na kukupeleka eneo lingine la kimaisha.
Kumb 1:6
"BWANA, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mlivyokaa katika mlima huu vyatosha"
๐Kama upo na Mungu katika maisha yako jua ya kuwa kufika lazima ufike sawasawa na kusudi la Mungu (Mungu atakuinua, kwenye elimu yako utavuka).
✍Wapo watu hukata tamaa kabisa kiasi ambacho hushindwa kuomba, hushindwa kufanya walichokuwa wanafanya kwa sababu wapo jangwani lakini pia wanachokiona jangwani kinawatia hofu ya kuendelea Mbele.
๐ถ♂๐ถ♀Kitendo cha wewe kupita jangwani(kwenye hiyo shida) ni kwa muda tu haupaswi kukata tamaa ila unapaswa kumtazama sana Yesu aliyekutoa hatua fulani ya kimaisha(kielimu,afya,biashara nk) ili akufikishe salama hatua nyingine ya kimaisha.
Kumb 8:2
"Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arobaini katika jangwa, ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo"
➡Baadhi ya watu hushindwa kumtazama Mungu hasa wanapopitia jangwani matokeo yake humkosea Mungu au humsahau Mungu aliyewatoa na kuwalinda kwenye kipindi fulani cha maisha kuwa anaweza pia kuwaokoa hapo jangwani.
๐ซ Wakati mwingine unaweza kuanza safari yako salama pamoja na rafiki zako unaowapenda na wanao kupenda.
๐Ila ukifika jangwani tena jangwa kubwa (shida kwenye biashara, Masomo, afya nk) wengi huweza kukukimbia ukabaki peke yako unateseka jangwani.
✍Kipimo cha rafiki sahihi kwenye maisha yako ni pale unapopitia kwenye shida ndipo utakapojua huu ni mchele na haya ni mawe.
๐Wapo marafiki wanaokuja kwako kwa sababu tu unavitu ila siku ukifirisika au kuishiwa na hao marafiki nao hupotea.
๐ Unapoanza safari yoyote ile (jambo lolote lile biashara, mtihani nk) hakikisha unaanza na Bwana unapokuwa safarini haijarishi utakutana na nini jangwani ila hakikisha unaendelea na Bwana ili ufike na Bwana safari yako iwe na Baraka za Mungu.
➡Utakapopita jangwani salama (elimu, ugonjwa nk) usije ukamsahau Bwana aliyekutoa Misri.
Kapayafarajaph@gmail.com
0768226595
Mungu akubariki sana
Comments
Post a Comment