MAOMBI
SOMO: USIACHE KUOMBA AU KUMWABUDU MUNGU KWA SABABU TU HAJAKUJIBU MAOMBI YAKO
Mwl: Fredrick kapaya
E-mail: Kapayafarajaph@gmail.com
Luka 18:1
Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa"
Mambo ya msingi
Mambo ya msingi
- Unawajibu wa kuomba au inakupasa umuombe Mungu siku zote haijarishi amekujibu maombi au hajakujibu maombi yako.
- Usiache kuomba au kwenda maombi au kanisani kwa sababu tu unaona kama vile Mungu hakujibu maombi unayoomba.
- Katikati ya hiyo hali ambayo unaona haiwezekani ila ndipo Mungu hujidhihirisha na kufanya mambo makuu.
- Elewa ya kuwa upo wakati ambao Mungu atakuondolea aibu uliyonayo, usichoke kusubiri
Kwenye hili somo tutaenda kuangalia baadhi ya mifano kutoka kwenye maandiko ili itusaidie na kutujenga tujue cha kufanya tutakapo kutana na hali za namna hii
Mfano wa kwanza:
Luka 1:5-13
"Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elesabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila
"Zamani za Herode, mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake Elesabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na maagizo yake bila
lawama. Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana. Basi ikawa, alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele za Mungu, kama ilivyokuwa desturi ya ukuhani, kura ilimwangukia kuingia katika hekalu la Bwana ili kufukiza uvumba. Akatokewa na malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia. Zakaria alipomwona alifadhaika hofu ikamwingia. Lakini yule malaika akamwambia, usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana"
Biblia inasema kuwa Zakaria na mkewe walikuwa ni watu wenye haki mbele za Mungu, inamaana walikuwa wakimuheshimu Mungu siku zote, lakini hawakufanikiwa kuwa na mtoto mpaka wamefika katika hali ya uzee wote wawili.
Yawezekana kuna watu waliwacheka, waliwabeza, waliwanenea maneno mengi kwa sababu ya kutokuwa na watoto pamoja na utumishi wao, lakini pamoja na hayo yote Zakaria na mkewe hawakumuacha Mungu kabisa bali waliendele kumtumikia Mungu siku zao zote.
Na ukisoma vizuri hapo utaona kuwa Zakaria aliendele kufanya kazi yake ya ukuhani na kuwahudumia watu wengine. Yawezekana alikuwa akipeleka shida za watu mbele za Mungu ili Mungu awasaidie hao watu, ndani yake bado alikuwa anamuamini Mungu kuwa anaweza hata kama hajawajibu maombi yao.
Elewa kuwa hata kama majibu ya maombi yako yamechelewa maadamu umeendelea kukaa kwenye uwepo wa Mungu, wakati wako wa majibu yako kuja ukifika hakuna atakayeweza kuzuia hata kama mazingira hayataruhusu ila lazima utapokea katika Jina la Yesu. Katikati ya ibada aliyokuwa akifanya Zakaria ndipo alipokutana na majibu ya maombi yake.
Elewa kuwa hata kama majibu ya maombi yako yamechelewa maadamu umeendelea kukaa kwenye uwepo wa Mungu, wakati wako wa majibu yako kuja ukifika hakuna atakayeweza kuzuia hata kama mazingira hayataruhusu ila lazima utapokea katika Jina la Yesu. Katikati ya ibada aliyokuwa akifanya Zakaria ndipo alipokutana na majibu ya maombi yake.
Hata wewe yawezekana kuna kitu umemuomba Mungu na bado hajakujibu, usiache mpendwa kumwabudu Mungu endelea kukaa kwenye uwepo wake ipo siku Mungu atakujibu na kuiondoa aibu yako kwenye maisha yako. Ukiondoka uweponi mwa Mungu utapishana na majibu au wakati wako wa kutembelewa na Mungu katikati ya shida yako.
Hebu piga picha: Je Zakaria angeacha kumwabudu Mungu na kufanya kazi ya makuhani yaani kuondoka katika uwepo wa Mungu angeweza kupokea majibu ya maombi yake? jibu ni hapana
Mfano wa pili
1 Samweli 1:1-19
"......Naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana na jina lake wapili Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto....."
Elkana alikuwa ni mtu ambaye alipenda sana ibada na maandiko yanasema kuwa alikuwa akienda kumwabudu Mungu na kumtolea sadaka Mungu huko Shilo, lakini pamoja na hayo mke wake Hana alikuwa hana mtoto, yawezekana Elkana na mke wake walikuwa wakimuomba Mungu sana juu ya swala hili kwa mda mrefu lakini hawakupokea majibu ya maombi yao. Pamoja na kutokupata majibu ya maombi hayo haikumfanya Elkana ache kwenda kumuabudu Mungu ila aliendele kwenda tena na tena, lakini pia hata Hana naye aliendelea kumuomba Mungu wala hakuacha kabisa.
Elewa kuwa chochote alichokikusudia Mungu kitokee juu yako lazima kitokee endapo tu utakuwa ndani yako ni mvumilivu lakini pia ukidumu katika uwepo wa Mungu huku ukikazana kumuomba Mungu siku zote pasipo kukata tamaa.
1 Samweli 1:15
"Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, nimeimimina roho yangu mbele za BWANA"
Wapo watu wamemuacha Mungu kwa sababu tu Mungu hajawajibu maombi yao waliyoyaomba kwa muda mrefu sana, wapo pia ambao hawana watotot kama Hana lakini wameshindwa kuumilia matokeo yake wamemuacha Mungu wa kweli wameenda kwa waganga wa kienyeji ili wapate majibu ya maswali yao.
Hata wewe unaweza ukawa na maswali ndani yam kichwa chako kuwa ni lini Mungu atafanya, nisubiri kwa mda gani mbona wakati unaenda? Ila inakupasa uelewe kuwa wakati ambapo unahisi kuchoka sana ndipo unapotakiwa kuelewa kuwa umekaribia kufika mwisho wako/ majibu ya maombi yako yamekaribia usiondoke ulipo.
Mfano wa tatu
Luka 18:2
"Akasema, palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini kwa kuwa mjane ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima"
Mwanamke huyu mjane alikuwa akimwendea huyu kadhi ili ampe haki yake, tena Biblia inasema kuwa alikuwa akimwendea-endea ina maana alienda mara nyingi kudai haki yake, alienda mara ya kwanza hakupa haki yke, hakukata tamaa alienda tena na tena, Ndugu yangu mpendwa yawezekana hata wewe kuna jambo unataka Mungu akutendee lakini bado hajakutendea kabisa, wapo wengine wamemwendea Mungu au wameomba Mungu bado hajawajibu kutokujibiwa kwao kumewafanya wakate tamaa. Sikiliza jambo kubwa la kujifunza kwa huyu mwanamke ni kuwa huyu mjane hakukata tamaa nasi tunatakiwa tusiwe watu wa kukata tamaa tunaposogea mbele za Mungu.
Luka 18:7
"Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao"?
Mungu akupe uvumilivu ndani yako katika jina la Yesu
Ubarikiwe sana
Comments
Post a Comment