Tambua jukumu ulilonalo
JIFUNZE NAMNA YA KUMPENDEZA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO
Mwl Fredrick kapaya
kapayafarajaph@gmail.com
Utangulizi
Watu wengi sana hupenda kukubalika mbele za watu kwa kile wnachokifanya u kwa tafsri nyingine watu wengi sana hupenda kusifiwa na watu baada ya kufanya jambo fulani, kwa hiyo upo uwezekano mkubwa wa mtu au watu kujibidiisha katika kufanya jambo fulani hata kama halipendi ili aweze tu kusifiwa au kuonekana mbele za watu kuwa anaweza na asipo sifiwa huweza kujisikia vibaya. Kama upo uwezo wa kufanya juhudi kwa ajiri ya kuwapendeza wanadamu basi tumia huo uwezo ndani yako kwa ajiri ya kumtafuta Mungu kwa juhudi lakini pia kuzitii amri zake kama ipasavyo ili usiwe chukizo mbele za Mungu bali Mungu apendezwe nawe.
Jambo la muhimu kujua ndani yako: Hauwezi kufanya jambo au mambo kiasi ambacho ukawapendeza wanadamu wote au watu wote hata kama jambo hilo ni zuri kiasi gani.
Jambo la muhimu kujua ndani yako: Hauwezi kufanya jambo au mambo kiasi ambacho ukawapendeza wanadamu wote au watu wote hata kama jambo hilo ni zuri kiasi gani.
Tambua ya kuwa unajukumu kubwa la kutafuta kumpendeza sana Mungu
Jukumu hili ni la muhimu sana, wengi sana wamesahau jukumu hili, akili zao na juhudi zao wameziweka katika kufanya mambo ya dunia hii kwa lengo la kuwapendeza wanadamu linaweza likawa sio jambo baya kwa namna moja. Ila kutafuta kuwapendeza wanadamu huku unavunja amri za Mungu ili tu uonekane mbele za watu hili ni jambo baya pia ni udhihirisho wa kuwa haumuheshimu Mungu lakini pia hauna msimamo kwenye imani yako.
Ukifanya huduma ya Mungu kwa lengo la kuwapendeza wanadamu wenzako ili wakuone kuwa nawe unaweza linaweza kuwa ni jambo la hatari sana kwa sababu upo uwezekano mkubwa wa kuwasikiliza watu nini wanataka kuliko kumsikiliza Mungu nini anataka afanye juu ya hao watu unaowahudumia lakini pia unaweza kutumia nguvu zako nyingi za kimwili kuliko kutumia nguvu za Rohoni.
Wagalatia 1:10
"Maana, sasa je! Ni mwanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo"
Paulo alikuwa mtumwa wa Kristo, kwa hiyo alijua jukumu lake ni kumpendeza Mungu/ kumtii /kumsikiliza Mungu aliyemtuma katika kazi hiyo ya utumishi wala si mwanadamu.
Mwanadamu ni muhimu sana ukajua kuwa uwapo hapa duniani hakikisha unafanya mambo mazuri au unakuwa karibu na Mungu huku ukimtii katika kufanya mambo yanayompendeza Mungu, sio kufanya mambo mabaya/machafu kwa ajiri ya kuwapendeza watu na kutafuta umaarufu usio kuwa na maana ambao hatima yake huwa mbaya.
Kumbuka kuwa Mungu amekuweka hapa duniani kwa kusudi, halafu kakupa jukumu la kufanya uwapo hapa duniani.
Mpendeze Mungu kwa sababu yeye ndiye mwenye kipimo sahihi cha kuweza kuuchunguza moyo wako na kujua nia ya moyo wako.
Kumbuka kuwa; Mungu
- Amekuweka hapa duniani
- Amekupa jukumu la kufanya
- Anakipimo sahihi cha moyo wako
1 Wathesalonike 2:4
"Bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu"
Amana ni kitu anachopewa mtu na mtu mwingine ili amtunzie au amwekee akiba kitu cha thamani hili ni jukumu
Mara nyingi sana wanadamu wanao tafuta kuwapendeza wanadamu wenzao ndani yao huwa na tabia ya kuhakikisha wanafanya wema usoni/ machoni pa watu ili waonekane kuwa ni wema mbele za watu, kumbe ndani yao hawako hivyo. Watu wa namna hii ni chukizo mbele za Mungu kwa sababu hiyo Mungu hapendezwi nao.
Mathayo 6:1
"Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao, kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni"
"Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao, kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni"
Matokeo ya kufanya wema au kutafuta kuwapendeza wanadamu kwa unafiki ni kukosa thawabu mbele za Mungu.
Biblia ya Habari njema inatoa tafsri nzuri ya neno thawabu.
"Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao, la sivyo Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo"
"Jihadharini msije mkafanya matendo yenu mema mbele ya watu kusudi mwonekane nao, la sivyo Baba yenu aliye mbinguni hatawapeni tuzo"
Yesu alikuwa anawaambia makutano kuwa waandishi na mafarisayo huwa na tabia ya kusema ila kiukweli hawatendi wanachokisema. Ina maana kuwa hutafuta sana kuwapendeza watu kuliko Mungu kwa sababu hiyo Mungu huchukizwa nao.
Mathayo 23:5
"Tena matendo yao yote huyatend ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao"
Unapokubari kusifiwa sana na wanadamu, inaweza kuwa si jambo baya ila ubaya wake unaweza kuwa kwa namna hii hasa kwenye huduma ya Mungu, unapozichukua hizo sifa kisha ukajiona ya kuwa wewe umefanya kwa nguvu zako yaani ukashindwa kumrudishia Mungu utukufu aliyekutumia wewe kufanya kilichofanyika (Kuponya waginjwa, wenye vifungo vya mapepo nk) kwa kufanya hivi unakuwa umemchukiza Mungu lakini pia haioneshi heshima yako kwa Mungu.
Mungu wetu angalii uzuri wako, ila anachoanza kaungalia kwanza ni moyo wako, haangalii maneno mengi unayo yaongea ila ana aangalia moyoni mwako je unamaanisha unachokisema?
Mungu wetu angalii uzuri wako, ila anachoanza kaungalia kwanza ni moyo wako, haangalii maneno mengi unayo yaongea ila ana aangalia moyoni mwako je unamaanisha unachokisema?
Mathayo 7:21
"Si kila aniambiaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, htukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, sikuwajua ninyi kamwe ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu"
Mwl Fredick Kapaya
Mungu wa Mbinguni akubariki sana
Comments
Post a Comment