SOMO: UWEZO ULIOPO NDANI YA CHANGAMOTO AU MATATIZO UNAYOPITIA


Mwl Fredrick kapaya 

E-mail: kapayafarajaph@gmail.com



  
Katika mfumo wa maisha ya mwanadamu, changamoto au matatizo ni mambo ambayo yapo na hutokea katika mazingira mbalimbali. Changamoto au matatizo huweza kuja katika sura za tofautitofauti sana, lakini pia tunaweza kuzitazama pia kwa namna tofauti tofauti hii ni kutokana na uwezo tulionao au uwezo ulio nao.

Wapo wengine kutokana na uwezo wao huishia kuzitazama changamoto au matatizo kwa sura ya nje kisha huingiwa na hofu sana, kubaki wanashangaa tu au hukata tamaa ya kuendelea mbele kwa sababu hiyo hizo changamoto husimama kama kizuizi kwao cha kuendelea mbele. Ila wengine huenda mbali zaidi na kuzitazama changamoto hizo kwa ndani zaidi kisha huona fursa, matumaini au hamasa ya wao kuzidi kusonga mbele zaidi au kuendelea kufanya wanachokifanya kwa bidii.

Ndani ya changamoto au matatizo huwa kuna uwezo fulani uliofichika mbele za watu au mtu kutokana na namna anavyoitazama hiyo changamoto au uwezo huo huweza kuonekana katika hali fulani. Uwezo huu ulio ndani ya changamoto anayopitia mtu au unayoipitia huweza kukupa wewe hamasa kubwa sana ndani yako katika kufanya unachokifanya au huweza kuua kilichondani yako au kukuzuia wewe usiweze kuendelea mbele.

Kutokana na tafsri ya neno changamoto, ndani yako unaweza kupata picha nzuri ya kukuonesha uwezo uliopo.

Changamoto: Ni hali ya kuwa na hamu ya kufanya kitu fulani , Desire to do something. Kwa hiyo zipo changamoto zinazokuja kisha huleta au kuongeza ndani yetu hamu ya kufanya jambo fulani kwa bidii. 

Changamoto ni jambo linaloweza kumuweka mtu njia panda. Changamoto huwa na uwezo wa kukufanya uchanganyikiwe yaani ushindwe kuendelea mbele.

Jambo la msingi sana: Ni muhimu sana ukaelewa kuwa si kila changamoto zinazokuja kwenye maisha yako huka kwa nia ya kukuangamiza au kukuweka njia panda ila changamoto zingine huja kwa nia ya kukusaidia au kukusukuma ili ufike unakotakiwa kufika ukiwa jasiri au kuamsha kile kilicho ndani yako ambacho hujawahi kukitumia lakini pia yawezekana haujui kama unacho (uwezo fulani) ili utumie au ukitumie kisha uvuke ulipo na ukishavuka ndani yako uwe na ufahamu wa kilichondani yako kisha ufanyike msaada kwa watu wengine.

Wakati mwingine unapopitia changamoto fulani usiwe mtu wa kulalamika sana, ni kweli kabisa zipo changamoto huweza kukuumiza sana, kukufanya ukate tamaa lakini wewe elewa kuwa wakati mwingine hizo changamoto huja kwa makusudi au kusudi la kukuimarisha huko unakoenda ili uwe mshindi au zinakuja kwa nia ya kukukomaza kiimani.

Au zinakuja ili kukuandaa uwe mtu fulani mkubwa kwenye eneo fulani, mara nyingi sana maandalizi ya mtu kufikia mafanikio makubwa hayawezi kuwa sawa na mtu wa kawaida tu. Wengi wanaopata mafanikio makubwa ni watu waliopitia changamoto nyingi kisha wakavumilia na hatimaye hufikia malengo yao. Changamoto alizokutana nazo Yusufu zilimuandaa kuwa mtu fulani.

Changamoto au matatizo ni darasa linaloweza kukupa mafundisho ili usikosee tena au usikosee lakini pia huwa na tabia ya kukuachia alama ndani yako au kwenye maisha yako. Hata kama utatuzi wa hiyo changamoto au tatizo ni mgumu basi hakikisha kuna kitu unajifunza ndani yake.

Hivyo basi hakuna kukataa changamoto bali unahitaji changamoto ili uweze kusonga mbele kuielekea ndoto yako.

Mungu wa mbinguni akubariki sana.

Comments

Popular posts from this blog

HATIMA YAKO

UAMINIFU

NAFSI ILIYOINAMA