SOMO: NGUVU ZILIZOPO NYUMA AU NDANI YA ZAWADI AMBAZO MTU HUPEWA








Mwl Fredrick Kapaya

E -mail: kapayafarajaph@gmail

Mwanzo 43:25

"Wakaiweka tayari ile zawadi hata atakapokuja Yusufu adhuhuri, maana wamesikia ya kwamba watakula chakula huko" 

Mambo ya msingi ndani ya hili somo:

  • Zawadi yoyote unayotaka kuitoa huhitaji maandalizi mazuri
  • Ni jambo zuri sana kupokea zawadi lakini pia umakini unahitajika sana ndani yake.
  • Unaweza kupokea zawadi lakini ndani yako usijue umuhimu au thamani ya hiyo zawadi uliyopewa.
  • Si jambo jepesi sana kukataa zawadi, kwa sababu hautaweza kueleweka vizuri kwa anayekupa zawadi hiyo.
Ila ikitokea Roho Mtakatifu kakupa maelekezo juu ya kutokupokea zawadi basi hakikisha unatii sauti hiyo.

Mfano: 

2 Wafalme 5:20

"Lakini Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akasema, Tazama, bwana wangu amemwachilia huyo Naamani Mshami, asivipokee mikononi mwake vile vitu alivyovileta...."

Baada ya Naaman kupona ugonjwa aliokuwa nao, Aliandaa zawadi ili kumpa Elisha zawadi hiyo ilikuwa inaonesha shukrani. Lakini Elisha hakukubali kuipokea hiyo zawadi ya Naamani, kutokupokea kwake Elisha zawadi hiyo kulikuwa na maana sana ndani ya Elisha.

lakini Gehazi , mtumishi wa Elisha hakujua sababu ya Elisha kutokupokea hiyo zawadi. Gehazi aliingiwa na tamaa juu ya ile zawadi kisha akaamua kurudi ili aichukue zawadi hiyo.

2 Wafalme 5:21-26

"Gehazi akamfuata Naamani. Naye Naaman alipoona......"

27. "Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele"

Zawadi ni kitu ambacho hupewa mtu au watu kwenye mazingira fulani. 

Zawadi ni kitu atunikiwacho mtu kuwa ni ishara ya upendo au pongezi kwa utendaji mzuri wa kazi fulani.

Ni kitu kinachotolewa na mtu kwa lengo jema (kushukuru, kupongeza, kuonesha upendo)

Ndani ya huu mchakato huwa kuna maeneo yafuatayo

  • Kinachomsukuma mtu kutoa zawadi
  • zawadi yenyewe
  • Anayetoa zawadi
  • Anayepokea zawadi
  • Namna anavyosikia anayepokea zawadi
 Mara nyingi sana kabla ya mtu kutoa zawadi yoyote ile ndani yake huwa kuna kitu kinachomsukuma au kuchochea kutoa. Kwa hiyo zawadi anayotoa mtu huwa na uhusiano mkubwa sana na kilichondani ya moyo wa mtu (zawadi inauwezo wa kuelezea kwa namna fulani kilicho ndani ya moyo wa anayetoa).

Elewa kuwa zawadi yoyote unayoipokea nyuma yake huwa na maana sana aidha kwenye ulimwengu wa roho au ndani ya moyo wa anayetoa. Au nyuma yake huweza kuambatana na nguvu fulani zenye uwezo wa kubadilisha moyo wako au kukuunganisha na madhabahu fulani za kiroho.

Ni jambo la muhimu sana kujua kuwa kila zawadi au zawadi nyingi sana huwa na maana sana kwa aliyeitoa au anayeitoa ingawaje kwako unaweza kuona kama ni kitu tu cha kawaida sana. Usipojua maana ya zawadi unayopewa au kupokea ni rahisi sana kufanyika mtumwa kwa anayekupa zawadi.

Unapokuwa na tabia ya kupokea zawadi basi ni muhimu sana kujifunza pia umuhimu wa kujua maana ya unachokipokea. Usipojua ipo siku unaweza kupokea visivyotakiwa kupokelewa nawe katika wakati huo.

Ndani ya zawadi huwa kuna nguvu zifuatazo. Hii hutegemea sana na nia ya mtoaji anayetoa hiyo zawadi.

  • Nguvu ya ushawishi au hamasa
  • Nguvu ya upendo au kuongeza upendo
  • Nguvu ya mabadiliko au kubadiri fikra za mtu
  • Nguvu ya kufanyika mtumwa wa aliyekupa zawadi
  • Nguvu ya umoja kati ya mtu na mtu 
  • Nguvu za kuteka nafsi ya mtu ili uweze kufanya jambo zuri au baya katika mazingira fulani. Nafsi yako inaweza kutekwa na kuwekwa kwenye kifungo au vifungo kutokana na zawadi unazopewa na mtu mwenye nia mbaya nawe.
Zawadi ni kitu chema sana ila ni muhimu sana ukajua au ukawa na ufahamu mkubwa kuhusu kuhusu kupewa zawadi kuliko kuwa na ufahamu tu wa kupokea na kusema asante.

Mungu wa mbingu akubariki sana
Mwl Fredrick kapaya
0768226595
Nzega, Tabora

Comments

Popular posts from this blog

HATIMA YAKO

UAMINIFU

NAFSI ILIYOINAMA