SOMO: TATIZO LINAWEZA KUWA SI KUONA UNACHOKIONA ILA LINAWEZA KUWA NI NAMNA UNAVYOONA UNACHOKIONA




Mwl Fredrick Kapaya

E-mail: kapayafarajaph@gmail.com



Waefeso 1:18

"Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo"

Kinachotusaidia sisi kuweza kuona ni macho yetu, yanaweza kuwa ni macho ya kimwili au kiroho. Macho ya kimwili au ya nyama hutusaidia kuona katika ulimwengu huu unaoonekana lakini macho ya rohoni hutusaidia kuweza kuona katika ulimwengu wa roho.

Lakini pia upo uwezekano mkubwa sana wa macho yetu kutiwa giza tusione tunachotakiwa kuona au tukaona vibaya mambo kwenye maisha yetu. Mara nyingi sana kwenye maisha tunaweza kushindwa kufanya mambo mengi sana kwa sababu tunayaona vibaya kwa sababu hiyo tunayatafsri katika namna ya kushindwa.

Mengine huja kwa sura ya matatizo kiasi ambacho tunapoyaangalia kwa macho yetu kwa juu juu huona ni matatizo ila wengine wakienda mbali zaidi katika kutazama huona ni fursa. Kinachoweza kukutofautisha wewe na watu wengine ni namna unavyoona mambo na kuyatafsri.

Lakini pia namna tunavyoyaona mambo ndivyo ambavyo tunaweza kutengeneza nafasi kubwa ya kushinda au kushindwa. Watu wengi sana walioshinda au kushindwa hawakuanzia hapo waliposhindwa au kushinda ila walianzia ndani yao namna walivyowaza, namna walivyoona au namna walivyoamua ndani yao kabla ya kutenda.

Ni ukweli usiopingika kwamba tunatofautiana sana namna tunavyoona mambo kwenye maisha

Mfano: 

Namna alivyoona Gehazi ilikuwa ni tofauti sana na namna alivyoona Elisha.

2 Wafalme 6:15

"Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, o;e wetu! Bwana wangu, tufanyaje"?  

Tunaingiwa na hofu sana kwa sababu ya namna tunavyoona mambo au changamoto. Wakati mwingie tunaona kama tuko peke yetu hakuna msaada kabisa. Gehazi namna alivyoona aliona jeshi la watu na farasi ghafla hofu iliingia ndani yake na aliona kabisa wanaagamia , kwa sababu macho yake yalikuwa yamefungwa. Kwa hiyo namna alivyoona kulifungua mlango wa hofu kuingia ndani yake.

Lakini  Elisha aliona tofauti na Gehazi ndio maana akamwambia hivi.

2 Wafalme 6:16

"Akajibu, usiogope, maana  walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao"

Kwa  sababu hiyo tatizo lililokuwepo kwa Gehazi kiasi ambacho aliingiwa na hofu lilikuwa si kwa kile alichokiona ila ni namna alivyoona kwenye yale mazingira.

2 Wafalme 6:17

"Elisha akaomba, akasema, Ee BWANA, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona BWANA akamfumbua macho yule mtumishi, naye akaona, na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote"

Kuna maeneo mangapi? kwenye maisha yako huingiwa na hali ya kukata tamaa au kuhisi una angamia , hofu inakujaa sana. Lakini ngoja nikutie moyo pamoja na hizo changamoto unazoziona ila wewe unatakiwa kuona kuwa upo msaada wa Mungu juu yako utakao kutoa ulipo. Usiogope kabisa.

Mungu akubariki sana
Mwl Fredrick kapaya
0768226595

Comments

Popular posts from this blog

HATIMA YAKO

UAMINIFU

NAFSI ILIYOINAMA