WEWE NI MSHINDI

Mwl Fredrick Kapaya

A prayer of Praise

Zaburi 27:3

_"Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijapotokea, Hata hapo nitatumaini"_
Plasms 27:3

_"Even if a whole army surrounds me, I will not be afraid; even if enemies attack me, i will still trust God"_
♦Katika ulimwengu wa roho lipo jeshi (jeshi la Mungu na shetani).
*Jeshi la Mungu*
*Luka 2:13*
"Mara walikuwapo pamoja na Huyo malaika, *wingi wa jeshi la mbinguni*,wakimsifu Mungu juu mbinguni"
*Luke 2:13*
"Suddenly a *great army of heaven's* angles appeared with the angle, singing praise to God"
*Jeshi la shetani (jeshi la pepo wabaya)*
*Waefeso 6:12*
"Kwa maana kushindana kwetu si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu was Giza hili, *juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho*
👉Jeshi   hili la shetani hujipanga ili kupigana na watu wa Mungu.

🔹Yawezekana yamejipanga kupigana nawe mpendwa ili kuhakikisha kuwa hauvuki hapo ulipo.
🚌 Kumbuka kuwa katika safari yako ya masomo, biashara au kuelekea kwenye hatima iliyobora, 🛣yawezekana njiani adui amejipanga ili kukuzuia usifike unakotakiwa kufika.
(Kajipanga katika ulimwengu wa roho pasipo wewe kujua kwa sababu anajeshi katika ulimwengu wa roho)
👂Sikiliza mpendwa wakati mwingine 👀ukiona changamoto zinazidi sana katika maisha yako elewa kuwa ndani yako kuna kitu cha thamani sana kwa sababu hiyo adui anafanya vita na wewe ili usikitumie ulichonacho, ili usipige hatua, ili ujidharau wewe mwenyewe au ukate tamaa.
_(Vita inapigwa juu yako sio kwa sababu ya umri wako, elimu yako, ila ni kwa sababu ya ulichokibeba ndani yako)_
⌚Wakati mwingine changamoto huja ili kukufanya ubaki unashangaa 🙆🙆‍♂kiasi ambacho utapoteza mwelekeo na kushindwa kuendelea mbele.🚶
📖Lakini pia katika andiko
*Zaburi 27:3* : kuna kitu tunaweza kukiona ndani yake, mara nyingi majeshi yanapojipanga ili kupigana vita.
👆👀Wengi wakiyaona majeshi hayo ndani yao huingiwa na hofu sana.
👂 Sikiliza nikwambie kitu ukiona ndani yako unaingiwa na hofu sana juu ya adui yako elewa kuwa ndani yako hauna uhakika na Mungu unayemwabudu.
🎤Daudi anasema kuwa "moyo wangu hautaogopa" Mara nyingi sana mtu ambaye ndani yake anaujasiri elewa kuwa nyuma yake huwa kuna kitu kinachompa ujasiri.
💪Daudi alikuwa jasiri kusema hivyo kwa sababu alikuwa na uhakika na Mungu aliyekuwa anamwabudu.
🏹Aliamini kuwa katikati ya vita upo ushindi lakini pia aliamini kuwa Mungu anayemtukia ana nguvu kuliko adui hata kama adui wako wengi kiasi gani. *,Ila akuangalia wingi wa adui Bali alitazama ukuu wa Mungu*_
🔹Daudi alipokutana na Goliathi hakuogopa.
*1 Samweli 17:45*
_"Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia Mimi na upanga na fumo, na mkuki, bali Mimi ninakujia wewe kwa jina La BWANA"_
🔹Ngoja nikwambie: Yawezekana watu walimuona Daudi kuwa ni dhaifu na hata Goliathi alimzalau kwa sababu aluona Daudi kuwa in dhaifu/hawezi kupigana.
*1 Samweli 17:42*
"Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi *akamdharau*
🔰Kuna watu wanakudharau namna ulivyo ila hawajui kuwa ndani yako una Mungu/wacha wakudharau yupo Mungu mwenye nguvu Mungu atakuheshimisha kwao nao watajua hakika upo na Mungu mwenye nguvu.
🔹Ukisoma vizuri habari za Daudi na Goliathi utagundua kuwa:
♦Daudi kiuhalisia alikuwa shujaa ndani yake ila alioneka kuwa ni dhaifu mbele za watu.
👆Goliathi alikuwa ni dhaifu kwa ndani Ila kwa nje alionekana kuwa ni shujaa mbele za watu kutoka na historia yake.
🔹 _U👕kitazama kwa jicho la rohoni_
👀Kwa sababu hiyo Daudi alipoangalia mbele yake hakuogopa (goliathi) kwa sababu ndani take alikuwa na Mungu aliyempa uhakika wa ushindi.
👉Yawezekana katika maisha yako kuna mifumo imetengenezwa na adui ili kusabisha ujione dhaifu au watu wakuone dhaifu kisha uingiwe na hofu.
🔸 Mwamini Mungu aliyendani yako usikaze macho yako katika kutazama shida iliyombele yako(goliathi) kisha ukaogopa.
🔰Ndugu yangu mpendawa yawezekana umeingiwa hofu na kupoteza matumaini kwa unachokiona mbele yako (jeshi) lakini ngoja nikutie moyo, haupaswi kuwa na hofu kwa unachokiona mbele yako.
🔰Kwa sababu Mungu wetu wa Mbinguini ni Mkuu kuliko kilichombele yako. Mungu wetu anauwezo wa kukusaidia kisha ukavuka hapo ulipo.
*Jione kuwa*:
👉Wewe ni jasiri
👉Wewe ni wa thamani
👉Wewe unanguvu
👉Wewe sio wa kubaki hapo ulipo.
Yesu anakupenda mno
*Ubarikiwe mno*

Comments

Popular posts from this blog

HATIMA YAKO

UAMINIFU

NAFSI ILIYOINAMA