NAFSI ILIYOINAMA Mwl Fredrick Kapaya October 2016 Nzega, Tabora Mithali 12:25 "Uzito wa moyo wa mtu huinamisha, Bali neno jema huufurahisha" Mwanadamu aliyeumbwa na Mungu amegawanyika katika mazingira au maeneo makubwa matatu ambayo ni mwili, nafsi na Roho. Nafsi ni eneo muhimu sana kwa sababu ni eneo linalohusika sana na kufanya maaamuzi ya mambo mbalimbali. Nafsi inaweza ikainama, kuinama kwa nafsi inamaana ya kupoteza matumaini ndani yako kutokana na mazingira uliyopo au unayoyapitia, au unapoona mbelea yako kama giza, wakati mwingine unafanya jambo na haufanikiwi inaweza fika eneo nafsi yako ikagoma kabisa. Shida au changamoto unazopitia zikizidi sana huwa na tabia ya kuweza kuilemea nafsi yako/kukulemea kiasi ambacho nafsi yako ikainama, ukashindwa kutazama mbele unakotakiwa kwenda kwa sababu hiyo akili yako na mawazo yako yote hukazana kufiri, kulitazama hilo gumu ulilonalo kwa mda mrefu. Mithali 12:25 "Uzito wa moyo wa...
Comments
Post a Comment