IMANI
“Basi imani ni kuwa na hakika ya mamboyatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” (Waebrania 11:1)
Kwahiyo tafsri ya Neno imani ni kuwa na hakika. Kila mtu kwenye maisha haya anaweza kuwa na imani ndani yake. Ila tunaweza kutofautiana tunachokiamini na namna tunavyoamini tunachokiamini.
Tunaishi hapa duniani kwa imani, katika kila jambo tunafanya kwa imani. Tunalala tunaamini tutaamka, tunalima tunaamini mazao yataota, tunakaa tunaamini hatuanguki, umekaa na rafiki yako unaimani ni mtu salama, tunaomba tunaamini Mungu atafanya, nk
“Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa
mbali na Bwana. (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona)” (2 Wakorintho 5:6-7)
Ili tujue kama imani iliyondani yako inafanya kazi maana yake tutaangalia matendo yako, “Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake” (Yakobo 2:17), Yakobo 2:5
Ukisoma Kitabu cha Timotheo, utaona Paulo alipokuwa amefungwa anamwandikia Timotheo kuwa alitamani sana kumuona lakini pia alikuwa anazungumza juu ya imani ya Timotheo. (2Timotheo1:3-6)“
Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana. Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha; nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako loisi, na katika mama yako Eunike, name nasadiki wewe nawe unayo. Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.
Katika hili andiko Paulo alikuwa anazungumza na Timotheo na baadhi ya mambo makubwa aliyokuwa anamwandikia ni kuhusu imani na karama iliyo ndani yake. Paul anaithibitisha imani aliyokuwa nayo
Timotheo kwamba ilikuwa ni imani isiyokuwa na unafiki na hii imani iliyo ndani ya Timotheo, PAUL
anasema kuwa aliiona kwa bibi lake loisi na kwa mama yake Eunike. Imani hii inaonekana ni imani ya kipekee sana kwa sababu Paul anajivunia kuiona imani ya namna hii. Yawezekana katika safari ya utumishi wa Paul aliona imani za namna nyingi ambazo zipo ndani ya watu au watoto wake wa kiroho.
Kama amezungumza kuhusu imani isiyo na unafiki maana yake aliona imani zilizokuwa naunafiki ndani yake, kama alizungumza kuhusu imani isiyo na unafiki maana yake kuna vitu vilivyomsaidia kujua kuwa imani ya Timotheo ni imani isiyo na unafiki.
Maswali
Je! Imani isiyo na unafiki ni imani ya namna
gani?
Imani yenye unafiki ni imani ya namna gani?
Ni vitu vipi vinaweza kutusaidia kujua kuwa
mtu Fulani anaimani ya kinafiki na mwingine
anaimani isiyo na unafiki?
Je imani inaweza kurithiwa.
Comments
Post a Comment